Latest News
U.S. President Obama Promotes HIV Testing
American President Barack Obama released a YouTube statement yesterday, asking Americans to get themselves tested for HIV. June 27th was the 14th annual National HIV Testing Day, launched in 1995 by the National Association of People With AIDS, an American NGO that was among the first to promote widespread testing.
It is estimated that one in five Americans, 250 000 people, living with the virus that causes AIDS, has not been tested.
The President’s YouTube address opens with video from an HIV testing drive he attended in Kenya in 2006, while a US Senator, where he and his wife were both tested for the virus. ”My wife and I are going to get tested for HIV/AIDS,” he told the crowd, “Because if you know your status, then you can prevent illness, you can prevent passing it to your children and to your families, and we can make everybody have happier, healthier lives.”
President Obama’s words echo PIUMA’s creed, Test and Live with Hope, and the work PIUMA has done in the past four years to promote HIV-testing and education in Bulongwa and its surrounding villages. PIUMA’s mobile testing campaigns have attracted hundreds of people to get tested and have allowed many to live better lives by providing support and information to those who are infected.
The President’s message from the White House yesterday was clear. ”HIV/AIDS makes no distinction and knows no borders,” he said. “Get tested. By knowing your HIV status, you can take control - not only of your own health, but the health of those around you.”
Gabe Maldoff
CARPENTARY WORK ON START!!
By Juma Nzige.
PIUMA building will be completed fitting of windows and doors after two months.Mr Izack Ngido who’s in charge for the carpentry work explained to the PIUMA leader about the progress on the preparation of windows, upper floor, and doors when the staff visited him at his site last week…
CANADIAN FRIENDS SUPPORTING PIUMA
By Juma nzige
Marafiki wa Canada wauwezesha mtandao wa PIUMA.
PIUMA website got support through some of Canadian friend. The donation aim to facilitate the programme of posting story in the website.
Handing over the sum of Tsh 600,000.00, The representative from Canadian friends Ms lucie Imbeau, told the general secretary about the anticipation of this money.
Stay in touch to www.piuma-simba.org
Bulongwa FC waichapa Mwakavuta Sekondari.
Na Evance Seth.
Michezo ni moja ya changamoto ya kupunguza maambukizi ya UKIMWI. Katika Wilaya ya Makete michezo huguswa sana na kupewa kipao mbele kuanzia shule za msingi, Sekondari hadi vijijini.
Katika mchezo wa mpira wa miguu uliochezwa siku ya Jumatano kati timu ya Mwakavuta Sekondari na Bulongwa football club katika uwanja wa Luvanyina maarufu kama Fly Emirates, ukiongozwa na refa bwana Aksoni Mahenge, timu ya Bulongwa football club (BFC) ilitoka na ushindi wa goli saba kwa moja dhidi ya timu ya Mwakavuta Sekondari.
Kwa kipindi cha kwanza cha mchezo Bulongwa football club ilifunga magoli mawili wakati Mwakavuta Sekondari ilitoka na goli moja, Katika kipindi cha pili cha mchezo Bulongwa football club waliongeza mashambulizi na kuibika na magoli manne na Mwakavuta sekondari kutoka bila goli. Hadi dakika ya mwisho ya mchezo Bulongwa football club ilitoka na ushindi wa magoli saba na wakati Mwakavuta sekondari ilitoka kwa goli moja.
Mwalimu wa michezo wa Mwakavuta Sekondari Bwana Robin Sanga hakuweza kuvumilia kipigo cha magoli hayo aliweza kuwaacha vijana wake uwanjani na kutoroka.
Kwani timu hizo zina upinzani wa hali ya juu, mechi ya kwanza Mwakavuta Sekondari ilishinda bao mbili kwa moja dhidi ya Bulongwa football club. Kapteni wa timu ya Mwakavuta alisema kuwa vijana wake kwa mechi hii wamecheza chini ya kiwango lakini hiyo ni moja ya mchezo, kwani mpira wa miguu una matokeo ya aina tatu, kufungwa, kufunga na kutoka droo.
Na wakati Kapteni wa timu ya Bulongwa football club Bwana Yotamu Nyasanga alisema kuwa vijana wake kwa mechi hii wamecheza mchezo mzuri kwani mechi ya kwanza walipofungwa wachezaji wake wengi hawakuwepo kufuatana na majukumu ya kimaisha.
Makapteni hao wote wawili walisema kwamba hii yote ni kupunguza maambukizi ya UKIMWI kwa vijana pamoja na kuviweka viungo fiti na kukwepa magonjwa nyemelezi.
Pamoja na michezo hiyo kuna baadhi ya matatizo mbalimbali wanayokumbana nayo timu zote mbili mojawapo ni vifaa vya michezo. Wachezaji wa Bulongwa football club walisema wanachotaka huko mbele waje kushiriki ligi kuu ya Tanzania bara.
Jezi ya Bluebahari ni timu ya Bulongwa FC na Nyeusi Mwakavuta Sekondari.
Mtikisiko wa uchumi wa Dunia kuokolewa na biashara ya Ulanzi!!
Na Evance Seth.
Pamoja na uchumi kuyumba kidunia wananchi wa Makete hawajakata tamaa katika utafutaji wa maisha kwa kutafuta fedha kwa njia mbalimbali ambazo ni halali. Pombe ya kienyeji itokanayo na miti iitwayo mianzi imekuwa ni sehemu ya chanzo cha mapato kwa sehemu kubwa ya wanamakete.
Kutokana na ugumu wa maisha wananchi wengi wa Wilaya ya Makete wanajishughulisha na biashara ya ugemaji na uuzaji wa Ulanzi. Akizungumza na mwandishi wa habari hii Bwana Kenedy Kayamba mkazi wa kijiji cha Maturunga mmoja wa wagemaji wa ulanzi alisema kuwa yeye alianza biashara hii mwaka 2004.
Alisema kuwa alipewa urithi wa vitindi na babu yake “wakati babu bado yupo tulikuwa tunaenda wote kugema na kunifundisha jinsi ya kugema, alinifundisha jinsi ya kupanda alisema kuwa niwe nachomeka kitindi mshazari, niwe nagema mara mbili kwa siku asubuhi na jioni na kuosha mbeta kila baada ya siku mbili. Nilifuata masharti ya babu na hatimaye nikafanikiwa , mwanzoni nilikuwa nagema lita kumi kwa siku, siku zilivyokuwa zinazidi kwenda lita za ulanzi zikazidi kuongezeka na hatimaye kwa sasa nagema lita ishirini kwa siku” alisema Bw. Kayamba.
Aliendelea kusema kuwa biashara hii ni ya msimu kwani inategemea mvua , wakati wa masika ulanzi huwa mwingi lakini biashara yake huwa sio nzuri kwani lita moja huuzwa kwa shilingi mia mbili na wakati wa kiangazi lita moja huuzwa kwa shilingi mia tano.
Alisema kuwa kwa kuwa biashara ni mbaya wakati wa masika, kwa hiyo wanachokifanya kwa sasa ni kununua madumu mengi yenye mifuniko na kugema ulanzi kuujaza kwenye madumu hayo, baada ya hapo wanaenda kuyafukia kwenye chemichemi za maji au sehemu yanapopita maji kidogo kwa ajili ya kuuza kiangazi, Kwa hiyo wanapofukia madumu hayo chini ya ardhi ndio friji lao, kwani ulanzi unaweza kukaa kwa muda wa miezi zaidi ya mitano na ukawa bado mzuri.
Hata hivyo Bwana Kayamba alisema kuna matatizo mbalimbali ambayo huwa anayapata ni pamoja na kung’atwa na nyuki akiwahi kwenda kugema kwani nao huwa wanakuwa wamelewa. “Mpaka sasa hivi hatuna soko la uhakika la mazao ya ulanzi hatuwezi kuuza kwa faida” aliongeza Bw. Kayamba
Lakini pamoja na changamoto hizo alisema kuwa mipango yake ya baadaye ni kuongeza shamba la vitindi, na kuidumisha biashara yake iwe ya kudumu kwa kiangazi na masika, kwa kuvitunza vizuri vitindi vyake kwa kuvipalilia ili aweze kugema ulanzi hata wakati wa kiangazi.
Marafiki wa PIUMA kutoka Kanada, Canadians Friends of Higlandshope walikuwa nafikiria kutafuta njia rahisi itakayoweza kuwasaidia wakulima wa ulanzi kutengeneza utomvu mzito “syrup” kutokana na kuchemsha ulanzi. Kama teknolojia hii itafanikiwa wakulima wa ulanzi watakuwa wamekombolewa kwani wataweza kuuza kwa faida bidhaa na mazao ya ulanzi.
Bwana Kayamba akiwa anagema ulanzi.
Ufugaji wa Samaki.
Na Evance Seth.
Katika hali ya kawaida kwa mtu ambaye amefika Wilayani Makete hawezi kutegemea kusikia habari ya samaki wabichi pamoja na ukweli kwamba wilaya hii kuwa na utajiri wa mito mingi, mikubwa na inayotiririka mwaka mzima lakini ni vigumu kuhisi kuwepo kwa samaki.
Upatikanaji wa samaki ni mgumu kwa sababu wilaya hii ina milima mingi hivyo maji yake kutiririka kwa kasi kubwa kuelekea ziwa nyasa au bonde la usangu.
Kutokana na kujua umuhimu wa zao la samaki wananchi wa Wilaya ya Makete wameanzisha kilimo cha ufugaji wa samaki kwa njia ya Mabwawa. Akizungumza na mwandishi wa habari hii Bwana Ilomo mmoja wa wafugaji wa samaki hao alisema kuwa yeye alianza mradi wa ufugaji wa samaki mwaka 2005.
Alipokuwa akichimba hilo bwawa watu walimcheka sana kufuatana na sehemu yenyewe jinsi ilivyokuwa na ugumu, kwani palikuwa na chemichemi. Pamoja na kuwa hakuwa na mbegu ya samaki lakini aliendelea kuchimba hayo mabwawa mpaka yalipofika matano.
“Kwa bahati nzuri binti yangu alinitafutia mtaalamu wa samaki Bwana Lingambe toka kijiji cha Utanziwa ambaye alikuja kuangalia jinsi mabwawa yalivyochimbwa” alisema Bw. Ilomo. Mtaalam wa samaki Bw. Lingambe alipoona mabwawa hayo yanafaa kwa ufugaji wa samaki alimuuzia Bw. Ilomo mbegu wa samaki aina ya Pelege mia tatu, wakati huo mbegu mmoja wa samaki alikuwa anauzwa kwa shilingi mia moja.
Aliendelea kusema kuwa ulipotolewa mkopo kwa wajasiliamali kutoka kwa Mh. Jakaya Kikwete, alitaka kuongeza mtaji kwa kwenda kukopa mkopo huo, lakini kutokana na masharti kuwa magumu alishindwa kupata mkopo huo.
Bw. Ilomo ansema alihitaji mtaji zaidi kwa ajili ya kuongeza mbegu zingine, kununua mabomba pamoja na kuinua kingo za bwawa. “Nilihitaji kama shilingi milioni moja tu” aliongeza Bw. Ilomo huku akionyesha sura ya masikitiko. Lakini alipowasilisha maombi yake benki aliambiwa na watoa mikopo hiyo kuwa wanakopesha kuanzia shilingi laki tano tu, na hizo fedha zinatakiwa kulipwa ndani ya miezi sita, kwa hiyo alishindwa kupata fedha hizo.
Lakini hakukata tamaa alitafuta namna nyingine kuweza kupata pesa aliyoitumia kwa ajili ya kununulia vifaa vilivyokuwa vinahitajika kwenye mabwawa hayo. Kwa sasa ana samaki wengi, ambao huwa anavua kwa ajili ya kujipatia kitoweo pamoja na kuwauza, na samaki mmoja huwa anamuuza kwa bei ya sh. 500 – 1000.
Hata hivyo Bwana Ilomo alisema kuna matatizo mbalimbali ambayo huwa anayapata hasa maji yanapojaa sana samaki hutoka nje na kusababisha hasara kwake, ukosefu wa zana za uvuvi, kukosa elimu ya ufugaji na uvuvi, samaki kuliwa na ndege pamoja na fisimaji, mtaji bado haujitoshelezi na uhaba wa soko la samaki.
Pamoja na changamoto anazozipata alisema kuwa kwa sasa anatumia dawa ya Letside kuua ndege na fisimaji kwa kumpaka samaki aliyekufa na kumweka kando ya bwawa na ndege hao humla huyo samaki na huenda kufa.
Mwisho alisema kuwa lengo lake kuu ni kuongeza samaki wa aina zingine, kuelimisha jamii inayomzunguka juu ya ufugaji wa samaki, kwani tangu aanze kufuga hao samaki na kuuza amefanikiwa kujipatia fedha kwa ajili ya kujikwamua matatizo mbalimbali.
Katika tarafa za Magoma na Bulongwa wilayani humu wanachama wa PIUMA nao wamekuwa wakiendesha miradi ya ufugaji wa samaki kwa njia ya Mabwawa.
Mzee Ilomo akiwa kwenye mabwawa yake.
Mbao Zao la Kuu la Biashara Makete.
Na Evance Seth.
Zao la mbao linaweza kuwa ni zao mbadala la pareto ambalo lilikuwa ni zao la biashara wilayani Makete mpaka miaka ya tisini lilipotoweka kutokana na kukosekana kwa soko.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii mmoja wa wafanyabiashara hao Bwana Osea Mahenge alisema kuwa hapo miaka ya nyuma mpaka miaka ya tisini mbao zilikuwa zikipasuliwa kwa msumeno wa mkono, lakini kadri watu walivyokuwa wakizidi kuendelea kupasua wameweza kufikia kiwango cha kupasua kwa mashine za mbao.
Bw. Mahenge alisema kuwa alianza biashara hii mwaka 2005 hadi leo bado anaendelea na biashara hii, ananunua mbao kutoka kijijini Bulongwa kwa bei ya jumla kwa ubao mmoja sh. 1000 hadi 1200 na kuzisafirisha kwenda kuuza Makambako au Mbeya kwa bei ya sh. 2000 hadi 2500 kwa ubao mmoja, usafirishaji wake huwa anakodi gari kwa mwenye gari kwa gharama ya sh. 450,000 hadi 500,000 ambapo gari hilo hubeba mbao 500 hadi 600 na gharama za utengenezaji na mafuta ni juu ya mwenye gari.
Aliendelea kusema kuwa mbao zimewasaidia sana katika kuendeleza maisha kwani tangu aanze kuuza mbao amefanikiwa kujenga nyumba yake, kusomesha watoto pamoja na kujikwamua kimaisha matatizo mbalimbali.
Wilaya ya Makete ni wilaya ya pili kwa kuwa na miti mingi mkoani ringa baada ya wilaya ya mufindi. Tofauti na mufindi ambako kuna misitu ya serikali ya Sao Hill, misitu ya Makete ni Mali ya wenyeji. Na mazao ya mbao yanayoonekana Makambako na Njombe yanatokea Makete.
Hata hivyo bwana Mahenge alisema kuna matatizo mbalimbali ambayo huwa anayapata hasa wakati wa masika biashara huwa mbaya kutokana na mvua ambazo huwa zinanyesha mfululizo na kusababisha kuharibika kwa barabara na kusimama kwa biashara hii.
“Pamoja na ubovu wa barabara wakati wa masika lakini pia tunatatizo la mitaji ya kuweza kuendesha biashara kubwa” alisema bwana Mahenge. Wapasuaji na wachuuzi wa mbao wameshindwa kupata mitaji kutokana na biashara zao kuwa za kuhama hama kufuatana na uwepo wa miti.
Wakati ukataji wa miti kwa ajili ya mbao umeambatana na kusababisha mmomnyoko wa udongo, Bwana Mahenge alisema hilo sio tatizo kwa wilaya ya Makete kwasababu miti ya mkaratasi inayotumika kwa mbao sasa hivi imekuwa ikijizalisha yenyewe bila kupandwa.
Hata hivyo uongozi wa wilaya umeombwa kuongeza juhudi za kuhamasisha wananchi kupanda miti kwani uwezekano wa misitu kutoweka ni mkubwa endapo uvunaji utakuwa ni mkubwa na upandaji kutokuwepo kabisa.
Wananchi wengi wamepata ajira isiyo rasmi kutokana na biashara ya mbao, akizungumza na mtandao Mwanamke mmoja Rehema Nyamule alisema, “nimekuwa nikipata mahitaji yangu muhimu kutokana na pesa ninayoipata kama ujira kwa kusogeza mbao kutoka msituni mpaka barabarani”
Wananchi wa tarafa ya bulongwa walipoongea na mtandao huu walisema uongozi wa wilaya yetu uongeze kutoa elimu juu ya upandaji miti ya biashara kwani inawapa faida mbalimbali kama kuuza miti yenyewe, mbao pamoja na kuni. Na kwa vijana itawasaidia kwa maisha ya baadaye.
Tarehe 5 mwezi wa sita ni kilele cha siku ya mazingira sherehe zake huazimishwa kila mwaka kwa kupanda miti. Wananchi wa Makete hushiriki katika shughuri hizo kwa kupanda miti katika kaya na vitongoji vyao.
Kauli mbiu yetu inasema panda mti kabla hujakata mti.
Mmoja wa wafanyabiashara wa mbao akiwa na rafiki yake.
Mahindi Tegemeo Milimani.
Na Witness Ngumba.
Zao la mahindi linategemewa sana katika Wilaya yetu ya Makete kwani ni zao kuu la biashara pamoja na chakula .
Akizungumza na mwandishi wa habari hii mkulima wa kijiji cha Madihani Bwana Pitulasi Sanga alisema kuwa zao hili linategemewa sana katika Wilaya yao kwani linawapatia chakula pamoja na kuuza kwa ajili ya kujikwamua matatizo mbalimbali ya kimaisha.
Bw. Sanga alisema kuwa zao hili hulimwa kwa kutumia jembe la mkono na hulimwa msimu wa kiangazi, zao hili huchukua muda wa mwaka mzima kukomaa na kuvunwa, hulimwa mwezi wa sita na kuvunwa mwezi wa tano, kwa hiyo ni karibia mwaka mzima, kuna baadhi ya vijiji hupandia mbolea lakini kwa kijiji chao hupanda bila mbolea na palizi yake ni mara moja tu, zao hili halistawi vizuri baadhi ya sehemu kutokana na kukosa pembejeo za kilimo.
Aliendelea kusema kuwa hata uvunaji wake wanavuna kwa mikono lakini usafirishaji wake zamani watu wengi walikuwa wanajitwisha kichwani na kupekeka mazao nyumbani lakini siku zinavyozidi kwenda watu wamekuwa wakielimika kwa kufuga punda kwa ajili ya kuweza kuwasaidia kubeba mazao hayo kutoka shambani kuyapeleka nyumbani na hawa punda wakati mwingine wamekuwa wakiwasaidia kubeba mazao hayo kuyapeleka sokoni kwa ajili ya kuuza.
“Matatizo tuyapatayo katika kilimo cha zao hili ni ukosefu wa pembejeo za kilimo pamoja na biashara kwani wakulima wengi tumekuwa tunalima zao hili lakini hatuna
Soko la uhakika, kwa hiyo tunajikuta tunauza kwa bei ya hasara”alisema Bw. Sanga
Pamoja na mahindi wilayani Makete pia kunalimwa Ngano, njegere, maharage, viazi vitamu, viazi mviringo.
Mkulima akivuna mahindi
Punda akibeba mahindi kutoka shambani.
KIKUNDI CHA TUSAIDIANE CHA WANAWAKE KATA YA INIHO - MAKETE
Na Evance Seth
Kufuatia kuongezeka kwa ugumu wa maisha mwaka 2003 wanawake wa kata ya Iniho wilayani Makete walianzisha kikundi cha Tusaidiane chenye malengo ya kuwafanya wasaidiane wanapokuwa na shida.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hii alipotembelea kikundi hicho ili kujua jinsi wanavyosaidiana wanawake hao walisema kuwa, Lengo la kikundi chao ni kusaidiana katika matatizo mbalimbali, kama , kufiwa na ugonjwa. Kikundi cha Tusaidiane chenye wanawake wanachama mia moja na tatu (103), kinajishughulisha na miradi ya uzalishaji mali.
Katika miradi ambayo kikundi kinaiendeleza ni pamoja na kilimo cha mahindi, ngano, viazi na bustani za mboga mboga. Pamoja na kilimo pia wanatusaidiane wamekuwa wakiendesha biashara ndogo ndogo. Akina mama hao wamekuwa wakiendesha migahawa na pia kufanya kazi ya kununua na kuuza nyanya na vitunguu.
Alipouulizwa kuhusu matumizi ya mapato yatokanayo na miradi ya kikundi hiki mwenyekiti wa kikundi hiki Bi. Rehema Mbogela alisema pesa inayopatikana inawasaidia wanakikundi kujikimu kimaisha. “wakati ikitokea shida kwa mwana kikundi mwenzetu kama kufiwa , huwa tunachanga fedha, tunanunua sanda, tunagharamia gharama za jeneza, unga na kuni kwa ajili ya kumuona mwenzetu, na huwa tunasaidia kazi za msibani kama, kupika, kuchota maji na zingine zijitokezazo” alisema Bi. Mbogela.
Wanachama walipohojiwa faida za Umoja wao huo walisema umoja huo umekuwa na faida kubwa kwao kwani umewasaidia wakati wakiwa wagonjwa. “Mwanakikundi mwenzetu akiugua na kulazwa hospitali huwa tunachanga fedha na unga kwa ajili ya kwenda kumwona” alisema mama Janeth Mbogela mwanakikundi mwanzilishi. Wanakikundi huonana pindi ndugu zao wauguapo au kufariki, Mume, baba, mama na watoto, ni wandugu walio kwenye orodha ya ndugu wauguao wanaompa mwanakikundi kupata haki ya kuonwa. Kwa shida za ugonjwa wa ndugu mwanakikundi ataonwa mara tatu kwa mwaka kwa upande wa ugonjwa.
Akina mama hawa walieleza kuwa waliamua kuingiza mpango wa kupeana pole kwenye ugonjwa na misiba kwasababu kuna wakati mwingine mtu anapo pata shida huwa anakuwa hana fedha wala chakula ndani ya nyumba, kwa hiyo ilibidi utafutwe mpango utakaowapa nafasi ya kumsaidia mwanakikundi mwenzao. Ukosekanaji wa mahitaji muhimu wakati wa shida mbali mbali uliwasukuma wanawake kuunda kikundi cha kusaidiana. Wakiongea na mwandishi wetu wa habari wanakikundi hao walisema kuwa kikundi chao kimefanikiwa sana kwani kimewavuta wanawake wengi kujiunga nao.
Mwenyekiti wa kikundi Bi. Rehema Mbogela.













